Newcastle,England.
Goli la dakika ya 90 la mlinzi Paul Dummett limeipa Newcastle United sare ya magoli 3-3 dhidi ya Manchester United katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa usiku wa leo katika uwanja wa St.James Park,Newcastle.
Kabla ya hapo matokeo yalikuwa Manchester United 3 na Newcastle United 2.Magoli ya Manchester United yamefungwa na Jesse Lingard na Wayne Rooney na yale ya Newcastle United yamepatikana kupitia kwa Georginio Wijnaldum na Alexandar Mitrovic
kwa mkwaju wa penati baada ya kufanyiwa madhambi na Chris Smalling.
Kufuatia matokeo hayo Manchester United bado imebaki katika nafasi ya sita baada ya kufikisha pointi 34 huku Newcastle United ikiwa nafasi ya kumi na nane baada ya kufikisha pointi 18 katika michezo 21.
Matokeo mengine:
Aston Villa 1-0 Crystal Palace (Joleon Lescott).Villa imepata ushindi wa kwanza baada ya michezo 19 ya ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment