728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, January 11, 2016

    SAMATTA NAHODHA MPYA TAIFA STARS,CANNAVARO BYE BYE

    Dar es salaam,Tanzania.

    Straika nyota nchini Mbwana Samatta anayekipiga katika kikosi cha TP Mazembe, ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa kikosi cha Taifa Stars.

    Uteuzi huo unahitimisha zaidi ya miaka mitano ya unahodha wa Stars kwa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni nahodha wa Yanga pia Zanzibar Heroes.

    Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amesema Samatta ndiye nahodha mpya wa kikosi chake.

    “Samatta ndiye nahodha mpya wa Taifa Stars, haya ni mabadiliko ya kawaida kabisa,” alisema Mkwasa.

    Mara ya mwisho, Cannavaro aliiongoza Stars akiwa nahodha baada ya kufungwa mabao 7-0 dhidi ya Algeria katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAMATTA NAHODHA MPYA TAIFA STARS,CANNAVARO BYE BYE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top