Ndola,Zambia.
Klabu ya Azam FC imeendelea kuwa mwiba mkali huko Zambia katika michuano ya kimataifa inayoendelea nchi humo baada ya jana jumamosi kuilaza Chicken Inn ya Zimbabwe kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Levy Mwanawasa mjini Ndola.
Azam FC imejipatia mabao hayo kupitia kwa nahodha John Bocco,Kipre Tchetche na bao la kujifunga la Brian Juru huku Nickie Muchedeyi akiifungia bao la kufutia machozi Chicken Inn.
Kufuatia ushindi huo Azam FC itajitupa tena dimbani Februari 3 kuvaana na Zanaco FC katika mchezo wa fainali na mshindi atatangazwa bingwa wa michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment