London,England.
Chelsea imeungana na vilabu vya Arsenal,Manchester City na Manchester United kutinga hatua ya tano ya michuano ya kombe la Emirates FA Cup baada ya kuilaza timu ya daraja la kwanza ya Milton Keynes Dons kwa mabao 5-1.
Chelsea imejipatia mabao yake kupitia kwa kinda wake Bertrand Traore,Oscar Dos Santos aliyefunga mabao matatu [hat-trick] kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka huku winga Eden Hazard akimaliza ukame wa kucheza dakika 273 kwa kuifungia Chelsea bao la tano huku Darren Potter akiifungia MK Dons bao la kufutia machozi.
Katika mchezo wa mapema Everton imetoka kifua mbele baada ya kuifumua Carlisle kwa mabao 3-0 huko Brunton Park kupitia kwa Aruna Kone,Aaron Lennon na Ross Barkley
0 comments:
Post a Comment