728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 29, 2016

    NEMANJA VIDIC ASTAAFU SOKA

    Manchester, England.

    Mlinzi wa zamani wa Manchester United Mserbia Nemanja Matic amestaafu soka ikiwa ni siku chache tangu atemwe na Inter Milan.

    Akitangaza uamuzi huo leo Vidic,34 amesema majeraha aliyoyapata miaka ya karibuni pamoja na ugonjwa wa Hernia ndivyo vimefanya aachane na mchezo huo uliompa sifa na utajiri mkubwa.

    Pia Vidic amewashukuru makocha,wachezaji na wafanyakazi wa vilabu vyote alivyowahi kuvichezea. 

    Vidic alianza soka lake kwa kuichezea klabu vya Red Star Belgrade kisha Spartak Moscow,Manchester United na mwisho Inter Milan huku mafanikio makubwa akiyapata akiwa na Manchester United baada ya kutwaa mataji matano ya ligi kuu,matatu ya kombe la ligi na moja la ligi ya mabingwa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NEMANJA VIDIC ASTAAFU SOKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top