London,England.
Kiungo mpya wa Arsenal Mmisri Mohammed Elneny anaamini ujio wake katika klabu hiyo ya London utaleta mataji matatu msimu huu.
Elneny,23 aliyejiunga na Arsenal jana alhamisi kwa ada ya paundi millioni 5 akitokea FC Basel ya Uswisi amesema mchango wake utaiwezesha Arsenal kutwaa mataji ya ligi kuu,FA na ligi ya mabingwa Ulaya licha ya kuwa na mchezo mgumu dhidi ya mabingwa watetezi FC Barcelona.
Elneny anatarajiwa kuanza kuichezea Arsenal jumapili hii katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Stoke City huko Brittania.
0 comments:
Post a Comment