728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 02, 2016

    IGHALO AITOLEA NJE ATLETICO MADRID

    Watford,England.

    Straika wa Watford Mnigeria Odion Ighalo amekataa kujiunga na Atletico Madrid licha ya klabu hiyo Hispania kumfuata zaidi ya mara tano.

    Kwa mujibu wa gazeti la The Sun,Atletico Madrid ilikuwa tayari kutoa kitita cha £12m ili kumnasa straika huyo wa zamani wa Udinese ya Italia lakini imekutana na kigingi baada ya mkali huyo wa mabao kusema anataka kubaki England.

    Chanzo cha karibu na Ighalo kimesema Atletico Madrid ilikuwa tayari kumlipa mara mbili zaidi ya mshahara anaolipwa na Watford.

    MFUNGAJI BORA WA MWAKA 2015

    Odion Ighalo ndiye mfungaji bora wa mwaka nchini England baada ya mwaka 2015 kufunga mabao 30 ambayo ni mengi zaidi kufungwa katika ligi zote nne za nchi hiyo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: IGHALO AITOLEA NJE ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top