Madrid,Hispania.
KUFURU!!Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kuitumia kuuelezea mkataba unaotarajiwa kusainiwa kati ya kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Adidas na klabu ya Real Madrid.
Kutoka katika gazeti la Marca taarifa zinasema Real Madrid iko katika hatua nzuri ya kufikia makubaliano na Adidas ya kusaini mkataba mnono wa udhamini wa miaka 10 wenye thamani ya £1b na kuwa klabu yenye udhamini mkubwa zaidi duniani.
Katika mkataba huo unaotarajiwa kuanza kutumika mwaka 2020 Real Madrid itakuwa ikivuna £106m kwa msimu ikiuzidi kwa asilimia 40 mkataba uliosainiwa mwaka 2015 wa £75m kati ya Manchester United na Adidas.
Mkataba huo unaotatrajiwa kuifanya Real Madrid kuwa klabu tajiri zaidi dunia umetajwa kuwa na thamani zaidi ya mikataba ya vilabu vya Chelsea, Arsenal na Liverpool kwa pamoja.
Vifuatavyo ni vilabu 10 vyenye udhamini mkubwa zaidi katika soka duniani.
1. Real Madrid - adidas €140m (£106m,Miaka 10)
2. Manchester United - adidas €98m (£75m, Miaka 11)
3. Bayern Munich - adidas €80m (£60m,Miaka 15 )
4. Chelsea - adidas €39m (£30m,Miaka 10)
5. Arsenal - Puma €39m (£30m,Miaka 5)
6. Liverpool - Warrior €32m (£24m,Miaka 6)
7. Barcelona - Nike €32m (£24m, Miaka 10)
8. Juventus - adidas €26m (£20m,Miaka 8 )
9. Milan - adidas €23m (£18m, Miaka 10 )
10. Paris Saint-Germain - Nike €23m (£18m,Miaka 11)
0 comments:
Post a Comment