Mido
Cairo,Misri.
Klabu ya Zamalek imemteua Ahmed Hossam "Mido" kuwa kocha wake mpya muda mfupi baada ya kumtimua kazi Mbrazil Marcos Paqueta.
Kutimuliwa kwa Pagueta kumekuja baada ya bodi ya wakurugenzi ya Zamalek kufanya kikao cha dharura siku ya jumapili na kuamua kuachana na kocha huyo aliyeajiriwa Desemba 8,2015 akichukua nafasi ya kocha Jesualdo Ferreira.
Sababu ya kutimuliwa kwa Pagueta ambaye juzi jumamosi aliiongoza Zamalek kutoka sare ya 2-2 na Misr Lel Makasa imedaiwa kuwa ni muendelezo wa matokeo mabaya inayoendelea kuipata miamba hiyo ya Misri.
Mpaka anatimuliwa kazi Paqueta ameiongoza Zamalek kucheza michezo mitano.Ameshinda michezo miwili dhidi ya Haras El Hodood na Ghazi El
Mehalia,ametoka sare michezo miwili dhidi ya Petrojet na Misr Lel
Makasa kisha kufungwa na Al Geish.
Mido anarejea Zamalek kwa mara ya pili baada ya mwaka 2014 kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Misri (Egypt Cup) na kisha kutimkia klabu ya Ismailia ambayo aliachana nayo mwaka 2015.
Mbali ya Mido Zamalek pia imemteua nyota wake wa zamani Hazem Emam kuwa mkurugenzi wake mpya wa michezo akichukua nafasi ya Ismail Youssef.
Uteuzi mwingine:Mohamed Salah na Medhat Abdel-Hady wamekuwa makocha wasaidizi wa kikosi cha kwanza huku Ayman Taher akiteuliwa kuwa kocha wa makipa
Pagueta
0 comments:
Post a Comment