Liverpool,England.
Klabu ya Liverpool imeimarisha kikosi chake baada ya jioni ya leo kumsajili kwa mkopo wa miezi sita mlinzi wa kati wa QPR aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Southampton Muingereza Steven Caulker.
Caulker,24 aliyeanzia soka lake katika klabu ya Tottenham amejiunga na Liverpool ili kuziba mapengo yaliachwa na walinzi Martin Skrtel, Dejan Lovren na Joe Gomez walio nje ya uwanja wakiuguza majeraha waliyoyapata katika michezo mbalimbali ya ligi kuu England.
Mpaka sasa Liverpool imefanikiwa kusajili wachezaji wawili tangu dirisha la usajili Ulaya lilipofunguliwa baada ya wiki iliyopita kumsajili Marko Grujic kutoka Partizan Belgrade ya Serbia.
0 comments:
Post a Comment