London,England.
JUMAPILI ya wiki hii kiungo Mjerumani Mesut Ozil ataweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka ligi kuu ya England kuvaa viatu vipya vya Adidas Ace 16+ visivyo na kamba za kufungia wakati atakapokuwa akiichezea Arsenal itayokuwa nyumbani Emirates kumenyana na Chelsea katika mchezo wa ligi kuu England.
Ozil,27 ambaye ni balozi wa kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Ujerumani amesema viatu hivyo vitamuondolea kero ya kuhangaika kufunga funga kamba kitendo ambacho humpotezea muda.
Viatu hivyo siyo vigeni nchini Hispania kwani tayari vimeshaanza kuvaliwa na kiungo wa FC Barcelona Ivan Rakitic.
0 comments:
Post a Comment