728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, January 07, 2016

    TP MAZEMBE YAACHANA NA KOCHA ALIYEIPA UBINGWA WA AFRIKA

    Lubumbashi,Congo.

    Klabu ya TP Mazembe imetangaza kuachana na kocha wake mkuu Mfaransa Patrice Carteron.

    Taarifa kutoka katika mtandao rasmi wa klabu hiyo ni kwamba TP Mazembe imeachana na Carteron baada ya kushindwa kumshawishi asaini mkataba mpya baada ya ule wa sasa kufikia mwisho.

    Carteron,45 alijiunga na TP Mazembe mwaka 2013 baada ya kuiongoza Mali kushika nafasi ya tatu katika michuano ya mataifa huru ya Afrika.

    Mafanikio

    - Akiwa na TP Mazembe Carteron alifanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi ya Congo mwaka 2013 na 2014.

    - 2013,Carteron aliiongoza TP Mazembe kushika nafasi ya pili katika michuano ya kombe la shirikisho.

    - 2015,taji la klabu bingwa Afrika




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TP MAZEMBE YAACHANA NA KOCHA ALIYEIPA UBINGWA WA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top