Zurich,Uswisi.
MSHINDI!!Lionel Messi ameibuka kinara kwa mara nyingine tena baada ya leo usiku kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia [Ballon d'Or] kwa mwaka 2015 huko Zurich,Uswisi.
Messi,28 ametwaa tuzo hiyo ya tano ya dunia baada ya kupata asilimia 41.33 ya kura zote zilizopigwa huku Cristiano Ronaldo aliyeshika nafasi ya pili akiambulia asilimia 27.76 na nafasi ya tatu imekwenda kwa Neymar Jr aliyepata asilimia 7.86.
Mbali ya Messi nyota mwingine aliyetamba usiku wa leo ni mwadada wa Kimarekani Carli Lloyd.Lloyd ameibuka kinara kwa upande wa wachezaji wa kike baada ya kutangazwa mchezaji bora wa mwaka.
Tuzo ya kocha bora wa mwaka imeenda kwa Luis Enrique wa FC Barcelona baada ya kuwashinda Pep Guardiola na Jorge Sampaoli wa Chile.
Jill Ellis wa Marekani ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa upande wa soka la wanawake.
Kikosi:2015 FIFPro World XI
Kipa: Manuel Neuer
Walinzi: Thiago Silva, Marcelo, Sergio
Ramos, Dani Alves
Viungo: Andres Iniesta, Luka Modric, Paul Pogba.
Washambuliaji: Neymar, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo
0 comments:
Post a Comment