Dar es salaam,Tanzania.
WINGA mahiri chipukizi wa Azam FC Farid Mussa mapema wiki ijayo anatarajia kwenda Hispania kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Farid mwenyewe ni kuwa klabu ya Slovenia ya FC Olimpija Ljubljana ambayo itakuwa nchini Hispania kwa kambi na mazoezi imempa mwaliko wa kufanya nayo majaribio kwa muda wa siku kumi na ikiwa atafaulu itamsajili moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment