Manchester, England.
Manchester United inajiandaa kufanya usajili wa dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya kwa kumsajili straika Mnigeria Ahmed Musa anayechezea CSKA Moscow ya Urusi.
Kwa mujibu wa The Express Manchester United imemgeukia straika huyo mwenye mabao 10 mpaka sasa baada ya mpango wake wa kutaka kuhamia Leceister City kukwama kufuatia CSKA Moscow kukataa ofa ya £15m kutoka kwa vinara hao wa ligi kuu England ikisisitiza Musa ana thamani ya £18.9m
Manchester United kupitia kwa kocha wake mkuu Louis Van Gaal inahitaji kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji hivyo imemuona Musa ambaye ni nahodha wa Nigeria kama mtu sahihi.
0 comments:
Post a Comment