London,England.
Klabu ya Chelsea imeendelea kunenepesha akaunti yake baada ya leo hii kumuuza kiungo Mbrazil Ramires Santos do Nascimento kwenda klabu ya Jiangsu Suning ya China inayonolewa na nyota wake wa zamani Dan Petrescu kwa dau la £25m.
Ramires,28 ameihama Chelsea baada ya kuitumikia kwa miaka mitano na nusu tangu ajiunge nayo mwaka 2010 akitokea Benfica ya Ureno kwa dau la £18m na kufanikiwa kufunga magoli 34 katika michezo 251.
0 comments:
Post a Comment