Newcastle,England.
Klabu ya Newcastle United imeendelea kujiimarisha baada ya usiku wa leo kumnasa winga Andros
Townsend kutoka klabu ya Tottenham Hotspur kwa ada ya £12m.
Townsend,24 amejiunga na Newcastle United kwa mkataba wa miaka mitano na nusu baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Tottenham Hotspur kilicho chini ya kocha Mauricio Pochettino.
Kabla ya kumnasa Townsend ambaye atakuwa akivaa jezi namba 25 tayari Newcastle United ilikuwa imewanasa Henry Saviet na Jonjo Shelvey.
0 comments:
Post a Comment