728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, January 20, 2016

    LIGI KUU BARA:RATIBA YA LEO NA KESHO IKO HAPA

    Dar es salaam,Tanzania.

    Ligi Kuu ya Vodacom mzunguko wa 15 unatarajiwa kuendelea leo Jumatano kwa michezo mitano, na Alhamisi kwa michezo mitatu kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu katika mzunguko huo.

    Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,Maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha Simba SC, Ndanda FC watakua wenyeji wa Mbeya City kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.

    Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,Stand United watacheza dhidi ya Toto
    Africans kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

    Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, Mwadui FC watawakaribisha Kagera
    Sugar katika uwanja wa Mwadui, African Sports watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani jijini Tnaga, huku Young Africans wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI KUU BARA:RATIBA YA LEO NA KESHO IKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top