Dar es salaam,Tanzania.
Mbwana Samatta ‘Popa’ ameondoka usiku wa Januari 27 kuelekea Ubeligiji kujiunga rasmi na klabu ya Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubeligiji maarufu kama Belgian Pro League.
Akiwa tayari amesaini mkataba na klabu hiyo,Samatta alikuwa anasubiri ‘taa ya kijani’ kutoka kwa boss wa TP Mazembe Moise Katumbi ambaye mwanzoni alikuwa anaweka ‘kauzibe’ kutoa ruhusa kwa mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa
wachezaji wa ligi za Afrika kwenda kujiunga na klabu ya Genk.
January 28 (Alhamisi) Samatta atakuwa ameshawasili nchini Ubeligiji tayari kwa ajili ya kuanza majumu mapya kwenye klabu hiyo ya barani Ulaya
0 comments:
Post a Comment