Abuja,Nigeria.
Mbwana Samatta ameandika historia mpya Tanzania na Afrika baada ya jana usiku kupata kura 127 na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka la ndani akiwashinda Robert Kidiaba wa Congo (Kura 88). na Baghdad Bounedjah wa Algeria.(Kura 63)
Samatta ametwaa tuzo hiyo baada ya kuiongoza TP Mazembe kutwaa taji la tano la klabu bingwa Afrika huku yeye akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga mabao nane.
Mbali na Samatta,Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon nae ameibuka kinara baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa jumla wa Afrika akiwashinda Yaya Toure wa Ivory Coast (Kura 136) aliyeshika nafasi ya pili na Andre Ayew wa Ghana aliyeshika nafasi ya tatu.(Kura 126)
Aubameyang ametwaa tuzo hiyo baada ya mwaka 2015 kupachika mabao 43 akiwa na Gabon na Borussia Dortmund.Aubameyang anakuwa mchezaji wa kwanza anayecheza ligi ya Bundesliga kutwaa tuzo hiyo mara nyingi imekuwa ikienda kwa wachezaji wanaocheza ligi za Hispania,Ufaransa na England.
Washindi wengine
Mchezaji bora kijana:Victor
Osimhen (Nigeria)
Mchezaji anayechipukia:Etebo Oghenakaro (Nigeria)
Kiongozi bora wa mwaka: Abdiqani Said Arab (Rais wa chama cha soka cha Somalia/Makamu Rais CECAFA)
Tuzo ya Platinum/Heshima Muhammadu Buhari (Rais wa nchi ya Nigeria)
Tuzo ya Fair Play:Allez Casa (Senegal)
Klabu bora ya mwaka:TP Mazembe
Timu bora ya taifa ya wanaume:Ivory Coast
Timu bora ya taifa ya wanawake:Cameroon
Kocha bora wa mwaka: Herve Renard
Mwamuzi bora wa mwaka:Papa Bakary Gassama (Gambia)
Legends wa Afrika:Charles Kumi Gyamfi (Ghana) na Samuel Mbappe Leppe (Cameroon)
0 comments:
Post a Comment