London,England.
Klabu ya Chelsea imeendelea kujiimarisha baada ya leo kumsajili mlinzi Matt Miazga toka New York Red Bulls ya Marekani kwa ada ya £3.5m.
Miazga,20 amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kuichezea Chelsea baada ya kuichezea New York Red Bulls kwa mafanikio ambapo aliisaidia kutwaa taji la ngao ya hisani mara mbili huku mwezi uliopita akitangazwa mchezaji bora kijana wa mwaka wa Marekani.
0 comments:
Post a Comment