Watford,England.
Klabu ya Watford imeendelea kujiimarisha baada ya kumsajili kiungo Muhispania Mario Suarez toka Fiorentina kwa ada ya paundi millioni 4.
Suarez,28 amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kuichezea miamba hiyo ya Vicarage Road inayotesa ligi kuu England.
Kabla ya kutua Fiorentina msimu uliopita Suarez alikuwa sehemu ya kikosi cha Atletico Madrid kilichotwaa ubingwa wa La Liga mwaka 2014/2015.
0 comments:
Post a Comment