Rubavu,Rwanda.
Timu ya taifa ya Uganda (The Uganda Cranes) imeanza michuano ya kombe la CHAN kwa kusuasua baada ya leo kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na timu ya taifa ya Mali katika mchezo mkali wa kundi D uliopigwa huko Umuganda Stadium,Rubavu.
Erisa Ssekisambu na Farouk Miya waliifungia Uganda Morimakan Koïta na Hamidou Sinayoko wakifunga kwa upande wa Mali Hamidou Sinayoko.
Katika mchezo mwingine wa kundi D Zambia iliitambia Zimbabwe baada ya kuilaza kwa goli 1-0.Goli hilo lilipatikana dakika ya 57 kupitia kwa Isaac Chansa.
Michuano hiyo itaendelea tena siku ya jumatano kwa michezo ya kundi A kupigwa ambapo wenyeji Rwanda watavaana na Gabon kabla ya Ivory Coast kuvaana na.Morocco.
0 comments:
Post a Comment