728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 30, 2016

    LIGI KUU BARA:SIMBA IKO DAR,YANGA TANGA,RATIBA NZIMA YA LEO NA KESHO IKO HAPA

    Dar es salaam,Tanzania.

    Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguko wa 16 kwa kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala salama.

    Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Simba SC watawakaribisha African Sports, JKT Ruvu watawakaribisha Majimaji
    FC uwanja wa Karume, huku Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Stand United kwenye uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

    Jijini Tanga, Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Young Africans uwanja wa Mkwakwani, Mwadui FC watakua wenyeji wa Toto Africans uwanja wa Mwadui Complex,huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakicheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja
    wa Kambarage mjini.Shinyanga.

    Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa mchezo mmoja ambapo Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribsiha Ndanda FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI KUU BARA:SIMBA IKO DAR,YANGA TANGA,RATIBA NZIMA YA LEO NA KESHO IKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top