728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 16, 2016

    HIDDINK AKIRI CHELSEA INAWEZA KUSHUKA DARAJA

    LONDON,ENGLAND.

    Uwezekano wa kilabu ya Chelsea kushushwa hadi daraja la kwanza la ligi kuu ya Uingereza upo,kaimu mkufunzi wa kilabu hiyo Guus Hidink amesema.

    The Blues wako katika nafasi a 14,ikiwa pointi sita juu ya timu tatu zinazokabiliwa na tishio la kushushwa katika ligi hiyo,na inatarajiwa kuchuana na Everton na Arsenal katika mechi zinazofuatia.

    ''Ni Kweli'',alisema Hiddink,ambaye alichukua timu hiyo kutoka kwa kocha Jose Mourinho mnamo mwezi Disemba.

    ''Tuna mechi mbili ngumu zinazofuata.Iwapo hutapata pointi za kutosha,hujui wengine watafanya nini.Ligi ya Uingereza inaweza
    kukushangaza''.

    Chelsea ilikuwa pointi moja juu ya timu tatu zinazokabiliwa na tishio la kushushwa daraja wakati Mourinho alipoondoka.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIDDINK AKIRI CHELSEA INAWEZA KUSHUKA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top