BARCELONA,HISPANIA.
CHAMA cha soka cha Hispania kimemfungia michezo miwili mshambuliaji wa FC Barcelona Luis Suarez baada ya kumkuta na hatia ya kuwaporomoshea mvua ya matusi wachezaji wa Espanyol katika mchezo wa jumatano wa hatua ya 16 wa kombe la Copa del Rey uliofanyika katika uwanja wa Nou Camp na FC Barcelona kushindwa kwa mabao 4-1.
Kufuatia adhabu hiyo Suarez atakosa mchezo wa marudiano utakaopigwa siku ya jumatano usiku kisha atakosa mchezo mmoja wa robo fainali ikiwa FC Barcelona itafuzu.
Wakati huohuo FC Barcelona imesema itaikatia rufaa adhabu hiyo kwa madai kuwa nyota huyo hana hatia.Katika mchezo huo Espanyol ilimaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya nyota wake wawili kulimwa kadi nyekundu kwa utovu wa nidhamu.
0 comments:
Post a Comment