728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 01, 2016

    CHICHARITO AZIDI KUMTUKANA VAN GAAL ATWAA TUZO YA PILI BUNDESLIGA

    Munich,Ujerumani.

    Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa yuko Bayer Leverkusen Mmexico Javier Hernandez Chicharito ameibuka tena kinara baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba wa ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga baada ya kufunga mabao saba katika michezo mitano iliyopita.

    Hii ni mara ya pili kwa Chicharito,27 kutwaa tuzo hiyo tangu atue nchini Ujerumani mwezi Julai mwaka jana baada ya kutupiwa virago na kocha Louis Van Gaal kwa madai kuwa hakuwa na jipya katika kikosi cha Manchester United.

    Mpaka sasa Chicharito ameifungia Bayer Leverkusen mabao 19 katika michezo 22 ikiwemo hat-trik dhidi ya Borussia Monchengladbach.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHICHARITO AZIDI KUMTUKANA VAN GAAL ATWAA TUZO YA PILI BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top