London,England.
Nahodha John Terry ametangaza kuachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu baada ya klabu hiyo ya London kugoma kumpa mkataba mpya pindi ule wa sasa utakapoisha mwezi juni.
Terry,35 ambaye ameichezea Chelsea kwa miaka 18 akiifungia mabao 66 katika michezo takribani 700 na kutwaa mataji manne ya ligi kuu,mataji matatu ya kombe la ligi na moja la ligi ya mabingwa ametoa tamko hilo baada ya leo hii kuiongoza Chelsea kuilaza MK Dons kwa mabao 5-1 katika mchezo wa raundi ya nne wa kombe la FA.
Akifanya mahojiano na Sky Sports,Terry amedokeza kuwa hatatundika daluga zake na badala yake atafikiria kucheza Marekani.
0 comments:
Post a Comment