Zanzibar
Yanga imetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya usiku wa leo kuitandika Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika mchezo mkali wa kundi B uliopigwa katika dimba la Aaman.
Mtibwa Sugar ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 10 kupitia kwa Shiza Kichuya.
Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Yanga ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 41 baada ya mpira wa adhabu wa Issoufou Boubakar kwenda moja kwa moja langoni mwa Mtibwa Sugar.
Dakika ya 81 Malimi Busungu aliifungia Yanga bao la pili akiunganisha kwa kichwa krosi safi ya Simon Msuva.
Dakika ya 86 Mtibwa ilipata pigo baada kiungo wake Henry Joseph kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Simon Msuva.
Kufuatia ushindi huo Yanga imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kufikisha pointi saba huku Mtibwa Sugar ikifuatia baada ya kuwa na pointi nne baada ya kushuka dimbani mara tatu.
0 comments:
Post a Comment