Mtwara,Tanzania.
Simba SC imewapa mashabiki wake zawadi ya mwaka mpya baada ya leo jioni kuilaza Ndanda FC kwa bao 1-0 katika mchezo wa kiporo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Nangwanda,Mtwara.
Bao lililoipa ushindi Simba SC limefungwa kipindi cha pili dakika ya 81 na mshambuliaji kinda Ibrahim Ajibu.
Kufuatia ushindi huo Simba SC imechupa mpaka nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara bada ya kufikisha pointi 27.
0 comments:
Post a Comment