Barcelona,Hispania.
Chama cha soka cha Ulaya (UEFA) jana ijumaa kilitoa orodha ya wachezaji XI waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2015.
Katika orodha hiyo ambayo hupatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki kupitia tovuti ya Uefa.com mabingwa wa Ulaya FC Barcelona wameibuka kidedea baada ya kutoa wachezaji watano wakifuatiwa na Real Madrid yenye wachezaji watatu huku Bayern Munich ikitoa wachezaji wawili na Juventus ikitoa mchezaji mmoja.
Wakati huohuo Cristiano Ronaldo ameweka rekodi baada ya kuingia kwenye kikosi hicho kwa mara ya kumi mfululizo huku ligi kuu ya Uingereza yenye wachezaji wakali kama Wayne Rooney,Eden Hazard na Mesut Ozil ikishindwa kutoa mchezaji hata mmoja.
KIKOSI KAMILI
Mlinda mlango: Manuel Neuer (Bayern Munich and
Germany).
Walinzi: David Alaba (Bayern Munich/Austria), Sergio Ramos (Real Madrid/Spain), Dani Alves (Barcelona/Brazil),Gerard Pique (Barcelona/Spain).
Viungo: Andres Iniesta (Barcelona/Spain), Paul Pogba (Juventus/France),
James Rodriguez (Real Madrid/Colombia).
Washambuliaji: Lionel Messi (Barcelona/Argentina) Neymar (Barcelona/Brazil)
na Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal).
0 comments:
Post a Comment