728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, January 27, 2016

    SIMBA YATAKA LIGI KUU BARA IBORESHWE


    Dar es salaam,Tanzania.

    Klabu ya Simba inatarajia kuwasilisha barua yake makao makuu ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kutoa tahadhari ambayo inaweza kuikumba ligi kuu Tanzania bara.

    Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo msemaji mkuu wa klabu ya Simba Haji Manara alisema “
    Imetustusha sana kuona kwamba TFF imetoa ruhusa kwa klabu kuweza kuacha kucheza michezo ya ligi yetu kuu na kwenda kucheza katika mashindano mengine ambayo hayakuwamo kwenye ratiba. Si tu kuwa imetushtusha ila pia ni uvunjifu wa katiba ambayo ndio inayosimamia ligi nzima “
    Sisi tutapeleka barua TFF kwa ajili ya kuelezea msimamo wetu kama klabu kwamba:

    1. Ligi kuu isiahirishwe, kwani kwa sasa hakuna
    klabu nyingine inayoweza kuomba udhuru katika kucheza mechi zake kwakuwa katiba inaitaka klabu yoyote kuomba ruhusa/udhuru siku 6 kabla ya kufika kwa mchezo wake unaofuata.

    2. Tutakapofika katika round 20 basi siku hiyo timu zote ziwe zinakamilisha mchezo wao wa 20 na sio wengine wapo mechi ya 19 au pungufu ya hapo. Hilo halitakubalika kwani kutakuwa na mianya ya kupanga matokeo.

    3. Ni vizuri sheria za TFF zikafuatiliwa kwa umakini mkubwa kwani katika kukosea kufanyia kazi moja ya sheria katika katiba yetu inayoongoza ligi kutasababisha migogoro isiyo na lazima kwenye ligi yetu.

    Mwisho kabisa napenda kuwatakia uongozi mzima wa TFF kazi njema na kuendelea kusisitiza kufuatwa kwa sheria zinazosimamia
    ligi yetu, alimalizia msemaji wa Simba Haji Manara. SIMBA NGUVU MOJA


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA YATAKA LIGI KUU BARA IBORESHWE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top