Genk,Ubelgiji.
Klabu ya Genk ya UbelgijiWa kimefanikiwa kumsajili mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta kwa mkataba wa miaka minne (2016-2020) akitokea TP Mazembe ya Kongo.
Samatta,24 amejiunga na Genk na kukabidhiwa jezi namba 77 baada ya kuipa Mazembe ubingwa wa ligi ya mabingwa Afrika huku yeye akiibuka mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Genk iko katika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi kuu Ubelgiji ikiwa na pointi 36.
0 comments:
Post a Comment