Munich,Ujerumani.
Mabao mawili ya Mshambuliaji Mpoland Robert Lewandowski
yameiwezesha Bayern Munich itwae ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya nne
mfululizo baada ya leo jioni kuibuka na ushindiwa mabao 2-1 dhid ya Ingolstadt.
Lewandowski alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati
uliopatikana baada ya Frank Ribery kuangushwa kwenye eneo la hatari na nahodha
wa Ingolstadt Marvin Matip kasha kuongeza la pili huku lile la kufutia wachozi la
wenyeji Ingolstadt likifungwa na Mortiz Hartmann.
Kwa ushindi huo Bayern Munich imekuwa timu ya kwanza ya
Ujerumani kutwaa ubingwa wa Bundesliga mara nne mfululizo,jumla ikiwa ni mara 26.

0 comments:
Post a Comment