728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 07, 2016

    HII NDIYO YANGA BHANA YAWACHAPA WAANGOLA MBILI SAFI U/TAIFA

    Dar es salaam,Tanzania.

    YANGA SC imeendelea vyena kuipeperusha bendera ya Tanzania katika duru za Kimataifa baada ya leo jioni kuichapa Sagrada Esparanca ya Angola mabao 2-0 katika
    mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kufuzu hatua ya makundi ya
    Kombe la Shirikisho la soka Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Mabao yaliyopeleka furaha Jangwani yamepatikana kipindi cha pili kupitia kwa Simon Msuva na Matheo Antony.Msuva alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 72 akiunganisha krosi safi ya Geofrey Mwashiuya.

    Dakika ya 91 Matheo Antony aliifungia Yanga SC bao pili kwa shuti kali lilombabatiza mlinzi mmoja wa Sagrada na kutinga wavuni.

    Kwa matokeo hayo Yanga SC wanahitaji sare yoyote ile au ushindi katika mchezo wa marudiano ili waweze kutinga hatua ya makundi.

    Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi: Deo Munishi,Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub
    ‘Cannavaro’, Salum Telela/Mbuyu Twite dk46, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Malimi Busungu/Godfrey
    Mwashiuya, Amissi Tambwe na Deus Kaseke/Matheo Anthony.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII NDIYO YANGA BHANA YAWACHAPA WAANGOLA MBILI SAFI U/TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top