728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 07, 2016

    WABISHI MIDDLESBROUGH WAREJEA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MIAKA SABA YA KUSOTA CHAMPIONSHIP.


    WABISHI Middlesbrough wamerejea tena Ligi Kuu England baada ya kusota Ligi daraja la kwanza (Championship) kwa miaka saba hii ni baada ya leo jioni kutoka sare ya bao 1-1 nyumbani Riverside na wagumu Brighton & Hove Albion.

    Middlesbrough ambayo iliingia katika mchezo wa leo ikihitaji sare yoyote ile au ushindi ili irejee Ligi Kuu ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya Cristian Stuani kufunga bao murua dakika ya 19.

    Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha wageni Brighton & Hove Albion ambao walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 55 kupitia kwa Dale Stephens ambaye hakudumu sana uwanjani kwani dakika ya 59 alilimwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mshambuliaji Gaston Ramirez.

    Kwa matokeo hayo Middlesbrough imepanda Ligi Kuu ikiizidi Briton kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa,zote zina pointi 89.Hivyo ili  Brighton & Hove Albion nayo ipande Ligi Kuu itahitaji kucheza michezo ya mtoano dhidi ya Sheffield Wednesday na. Kisha dhidi ya mshindi kati ya Hull City na Derby County ili kukamilisha idadi ya timu tatu zinazotakiwa kupanda.

    Timu zilizopanda Ligi Kuu mpaka sasa ni mabingwa Burnley na Middlesbrough.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WABISHI MIDDLESBROUGH WAREJEA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MIAKA SABA YA KUSOTA CHAMPIONSHIP. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top