Norwich,England.
Manchester United imeendelea kupambana kurejea katika nafasi nne za baada ya mchana wa leo kuichapa Norwich City bao 1-0 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu England uliopigwa katika uwanja wa Carrow Road huko Norwich.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 72 ya kipindi cha pili na kiungo Juan Mata.Mata amefunga bao hilo akipokea pasi ya nahodha Wayne Rooney aliyeunasa mpira wa kichwa wa mlinzi wa Norwich City, Sebastien Bassong.
Matokeo hayo yanaiacha Manchester United katika nafasi ya tano,pointi moja chini ya Manchester City iliyo nafasi ya tatu na pointi nne ya West Ham United iliyo nafasi ya tano.Norwich City imebaki nafasi ya 19 pointi mbili juu ya mstali wa kushuka daraja.
VIKOSI:
Norwich: Ruddy, Ivo Pinto, Martin,
Bassong, Olsson, Redmond, O’Neil,
Howson, Brady, Hoolahan, Jerome
Akiba: Whittaker, Naismith, Mbokani,
Bamford, Rudd, Jarvis, Dorrans.
Man United: De Gea, Valencia, Smalling,
Rojo, Darmian, Carrick, Lingard, Mata,
0 comments:
Post a Comment