728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 07, 2016

    RONALDINHO MBISHI BHANA!!

    Sao Paulo,Brazil.

    LICHA ya kuwa na umri mkubwa wa miaka 36 nyota wa zamani wa Brazil Ronaldinho Gaucho amesema bado ana mipango ya kuendelea kucheza soka iwe nyumbani kwao Brazil ama kwingineko atakakohitajika.

    Ronaldinho ambaye amekuwa hana timu tangu mwezi Septemba mwaka jana alipotemwa na Fluminense amesisitiza kuwa safari yake ya kucheza soka bado haijafika mwisho na kuongeza kuwa anatarajia kusaka timu mpya katika dirisha lijalo la usajili.

    Akiongea kutoka Sao Paulo,Brazil amesema kwa sasa anajihusisha na shughuli za promosheni lakini katika nusu ya pili ya mwaka huu tutegemee kumuona akirejea tena dimbani.

    Ronaldinho hajapata tena bahati ya kucheza soka Ulaya tangu mwaka 2011 alipomaliza mkataba wake wa miaka mitatu na AC Milan.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RONALDINHO MBISHI BHANA!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top