728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 07, 2016

    MJUE MWAFRIKA KWA KWANZA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU ENGLAND NA WOTE WALIOMFUATIA,MIAKA NA VILABU WALIVYOCHEZEA

    Wreh

    London, England.

    Leo Jumamosi Leceister City inatarajiwa kukabidhiwa taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya mchezo wake dhidi ya Everton utakaopigwa huko King Power,Leceister mida ya jioni.

    Katika tukio hilo kubwa itashuhudiwa nyota watatu wa Kiafrika Ryad Mahrez Daniel Amartey na Jeffrey Schlupp wakiingia katika vitabu vya kumbukumbu ya kuwa sehemu Waafrika waliopata bahati ya kutwaa taji hilo lililoanza kugombaniwa tangu mwaka 1992.

    Je,Ni Waafrika wangapi wamefanikiwa kutwaa taji hilo kubwa nchini England??Nani wa Kwanza???

    Mliberia Christopher Wreh:Huyu ndiye Mwafrika wa kwanza kutwaa taji la Ligi Kuu nchini England.Wreh alitwaa ubingwa huo msimu wa 1997-98 akiwa na Arsenal iliyokuwa imemsajili toka Monaco ya Ufaransa.

    Katika msimu huo Wreh ambaye ni binamu wa nyota wa zamani wa Monaco,AC Milan na Chelsea,George Weah alifanikiwa kufunga mabao matatu kabla ya mwaka 2000 kuuzwa kwenda Al-Hilal ya Saudi Arabia.

    Mpaka leo hii jumla ya Waafrika 14 pekee ndiyo wamefanikiwa kutwaa taji hilo huku Didier Drogba akiwa kinara baada ya kutwaa taji hilo mara tatu akiwa na Chelsea.

    ORODHA KAMILI IKO KAMA IFUATAVYO

    1.Christopher Wreh | Liberia | Arsenal 1997-98
    2.Nwankwo Kanu | Nigeria | Arsenal 2001–02,
    2003–04
    3.Lauren Etame Mayer | Cameroon | Arsenal
    2001–02, 2003–04
    4.Quinton Fortune | South Africa | Manchester
    United 2002-03.
    5.Kolo Toure | Cote d'Ivoire | Arsenal 2003-04,
    Manchester City 2011-12
    6.Didier Drogba | Cote d'Ivoire | Chelsea 2004–
    05, 2005–06, 2009–10, 2014–15
    7.Geremi Njitap | Cameroon | Chelsea 2004–05,2005–06
    8.Michael Essien | Ghana | Chelsea 2005–06,2009–10
    9.Salamon Kalou | Cote d'Ivoire | Chelsea 2009-10
    10.John Obi Mikel | Nigeria | Chelsea 2009–10,2014–15.
    11.Yaya Toure | Cote d'Ivoire | Manchester City
    2011–12, 2013–14
    12.Riyad Mahrez | Algeria | Leicester City 2015-16
    13.Daniel Amartey | Ghana | Leicester City 2015-16
    14.Jeffrey Schlupp | Ghana | Leicester City 2015-16



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MJUE MWAFRIKA KWA KWANZA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU ENGLAND NA WOTE WALIOMFUATIA,MIAKA NA VILABU WALIVYOCHEZEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top