728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 07, 2016

    NYOTA MWINGINE WA CAMEROON AFIA UWANJANI

    Bucuresti,Romania.

    Kiungo wa kimataifa wa Cameroon Patrick Ekeng amefariki dunia Ijumaa usiku baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Romania uliokuwa unahusisha klabu yake ya Dinamo Bucuresti dhidi ya Viitorul Constanta ns kuisha kwa sare ya mabao 3-3.

    Ekeng,26 amefikwa na umauti huo dakika ya 70 ya mchezo zikiwa ni dakika saba tu tangu aingie uwanjani akitokea benchi. 

    Katika mchezo huo uliokuwa unarushwa live kwenye TV,tukio la Ekeng kuanguka limetokea wakati
    akiwa kasimama peke yake bila ya mpira.

    Taarifa za kifo cha Ekeng zimethibitishwa masaa mawili baada ya
    kufikishwa hospitali ya Floreasca Emergency Hospital.Sababu ya chanzo cha kifo cha nyota huyo wa zamani wa Mans,Lausanne na Cordoba kimedaiwa kuwa ni shambulio la moyo [heart attack].

    Hii ni mara ya pili kwa Dinamo Bucharest kukutwa na mkasa kama huo kwani mwaka 2000 aliyekuwa nahodha wake Catalin Hildan alianguka na kufariki dunia katika mchezo wa kirafiki.

    Vilevile hii pia ni mara ya pili kwa Cameroon kupoteza nyota wake uwanjani.Mwaka 2003 kiungo Marc-Vivien Foe alifariki dunia wakati akiichezea Cameroon katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la mabara dhidi ya Colombia,huko Ufaransa. 

    Ekeng alijiunga na Dinamo
    Bucharest, mwezi Januari mwaka huu na kufanikiwa kuifungia bao moja katika michezo saba aliyofanikiwa kucheza.Pia ameichezea Cameroon michezo saba ya kimataifa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NYOTA MWINGINE WA CAMEROON AFIA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top