728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 07, 2016

    RONALDO DE LIMA ASEMA "I SEE ME" AKIMTAZAMA RASHFORD.

    Rio de Janeiro,Brazil.

    Nyota wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima ameshindwa kuficha hisia zake na kuamua kumwagia sifa mshambuliaji kinda wa Manchester United Marcos Rashford,18 kuwa dogo anajua.

    Akifanya mahojiano na SunSport,Ronaldo aliyewahi kutamba na vilabu vya Barcelona, Inter Milan na Real Madrid amefichua kuwa kila anapomtazama Rashford anajiona yeye kabisa.

    "Ni mchezaji mzuri sana.Kila ninapomtazama namuona ana uRonaldo uRonaldo hivi ndani yake.Ni jasiri ana kasi na ni mzuri sana akiwa na mpira.Kitu muhimu kwa mshambuliaji yoyote yule ni kufunga mabao sifa ambayo Rashford anayo.Naamini atafika mbali".Alimaliza Ronaldo aliyeifungia Barcelona mabao 34 katika michezo 37 mwaka 1996 akiwa kinda wa miaka 20 tu.

    Rashford ameichezea Manchester United michezo kumi na tano na kufanikiwa kufunga mabao saba tangu alipooanza kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza na kocha Louis Van Gaal.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RONALDO DE LIMA ASEMA "I SEE ME" AKIMTAZAMA RASHFORD. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top