Jos,Nigeria.
Mlinda mlango wa klabu ya Giwa ya Jos,Nigeria Timothy Chichi Okere amefariki dunia kwa maumivu ya uti wa mgongo.
Timcy Baba kama alivyopenda kuitwa na wachezaji wenzake wa Giwa FC alipatwa na tatizo hilo mwaka 2014 baada ya kuumia mazoezi na kukazimika kulazwa katika Hospitali ya Bida kwa siku kadha kabla ya kuruhusiwa.
Ghafla tatizo hilo limejirudia tena wiki hii na kufanikiwa kukatisha uhai wake siku ya Alhamis.Kabla ya kutua Giwa FC,Timcy Baba alichezea Mighty Jets.
Giwa FC itamkumbuka Timcy Baba kwani alikuwa mhimili mkubwa katika kuipandisha daraja klabu hiyo mpaka ligi kuu ya Nigeria misimu mitatu iliyopita kabla ya kupoteza namba kikosi cha kwanza kwa Ojo Olorunleke.
0 comments:
Post a Comment