728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 06, 2016

    ALIYEMTIA KIDOLE CHA MACHO DIEGO COSTA AFUNGIWA MECHI SITA

    London,England.

    Chama cha soka cha England FA leo kimetangaza kumfungia michezo sita kiungo wa Tottenham Mousa Dembele baada ya kukiri kumtia kidole cha macho mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa.

    Dembele,28 alifanya kosa hilo Jumatatu ya wiki hii katika mchezo wa Ligi Kuu ulioisha kwa sare ya kufungana mabao 2-2 huko Stamford Blidge,Kusini mwa London.

    Hii ina maana kwamba Dembele atakosa michezo miwili iliyobakia ya kumalizia msimu huu ambayo ni dhidi ya Southampton na Everton kisha michezo mingine minne ya mwanzo wa msimu unaokuja wa 2016/17.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ALIYEMTIA KIDOLE CHA MACHO DIEGO COSTA AFUNGIWA MECHI SITA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top