MABINGWA watetezi, Kenya wamevuliwa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challege baada ya kufungwa na Rwanda kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 mjini Addis Ababa, Jumanne.
Amavubi sasa itakutana na Sudan katika Nusu Fainali, ambayo jana iliitoa Sudana Kusini kwa penalti 5-3 pia baada ya sare ya 0-0.
Ikumbukwe Robo Fainali za kwanza Jumatatu, Uganda iliitoa Malawi kwa kuichapa mabao 2-0, wakati Ethiopia iliitoa Tanzania kwa kuifunga penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Alhamisi, Uganda ikimenyana na wenyeji Ethiopia na Rwanda ikivaana na Sudan.
0 comments:
Post a Comment