Leceister,England.
Leceister City imeendelea kuwa kinara katika ligi kuu ya nchini England baada ya mshambuliaji wake Jamie Vardy na kocha wake Claudio Ranieri kutwaa tuzo ya mchezaji bora na kocha bora kwa mwezi Novemba.
Vardy ambaye ni kinara wa upachikaji mabao na mshindi wa tuzo hiyo kwa mwezi uliopita wa Octoba ameibuka tena kidedea kwa mwezi Novemba baada ya kuendeleza rekodi ya kupachika mabao kila kukicha na kuwabwaga Harry Kane,Ross Barkley,Troy Deeney, Romelu Lukaku na
Dejan Lovren.
Naye kocha Ranieri ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Novemba baada ya kuingoza Leceister City kumaliza mwezi Novemba bila kupoteza mchezo hata mmoja ikiwa imezifunga Watford na Newcastle huku ikienda sare ya 1-1 na Manchester United.
Ranieri ametwaa tuzo hiyo kwa kuwabwaga Jurgen Klopp, Everton’s Roberto Martinez na Mauricio Pochettino.
0 comments:
Post a Comment