Kampala,Uganda.
Emmanuel Okwi ameendelea kupachika mabao matamu kwenye michezo ya ligi kuu ya Uganda kama ilivyo kwa Mtanzania Mbwana Samatta anayetesa kwasasa nchini Ubelgiji akiwa na KRC Genk hii ni baada ya jana Jumanne kufunga bao moja na kuiwezesha SC Villa kuichapa The Saints mabao 2-0 katika mchezo mgumu uliochezwa kwenye uwanja uliojaa tope kutokana na mvua kubwa kunyesha huko Mwerwere.
Okwi ambaye amerejea Uganda hivi karibuni na kujiunga na SC Villa akiwa kama mchezaji baada ya mambo kumwendea kombo nchini Denmark,amefunga bao hilo kwa mkwaju mkali wa mbali katika dakika ya 64 ya mchezo na kufikisha mabao saba katika michezo saba.Bao la pili la SC Villa limefungwa na mlinzi wake wa kati,John Adriko.
Ikumbukwe Jumapili iliyopita Okwi aliibuka tena shujaa baada ya kuifungia SC Villa mabao matatu katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Onduparaka FC.
Matokeo ya michezo mingine ya Jana Jumanne
Express 4-3 Police
The Saints 0-2 SC Villa
Soana 1-1 JMC Hippos
BUL 2-0 Bright Stars
Sadolin 0-0 Lweza
0 comments:
Post a Comment