London,Uingereza
CHAMA cha soka nchini Uingereza ‘FA’ kimeituhumu klabu ya Manchester United kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Chelsea uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge jana na kama watashindwa kujitetea basi wataadhibiwa.
Tuhuma hizo zimetokana na kitendo cha wachezaji wa United kumzonga mwamuzi Michael Oliver katika dakika ya 35 baada ya kiungo Ander Herrera kuonyeshwa kadi ya Nyekundu kufuatia kumkwatua winga wa Chelsea Eden Hazard
Herrera alipewa kadi ya pili mbili ya njano zote zikiwa ni kumfanyia madhambi Hazard na kutolewa uwanjani huku wachezaji wa United wakimzingira mwamuzi wakipinga kadi ya pili aliyopewa mwenzao.
Mashetani hao wekundu wamepewa hadi Ijumaa jioni wawe wamejibu tuhuma hizo kabla FA haijatoa hukumu kwa kosa hilo.
Chelsea walifanikiwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya United pungufu likifungwa na kiungo mkabaji Ngolo Kante na kuweza kutinga nusu fainali ya michuano hiyo wakikutana na Tottenham Hotspurs mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment