Manchester, England.
KIUNGO wa Manchester United,Ander Herrera hataonekana uwanjani kwa kipindi cha majuma mawili hii ni baada ya chama cha soka England (FA) kumtwanga adhabu ya kukosa mechi mbili kwa utovu wa nidhamu.
Juzi Jumatatu Herrera alionyeshwa kadi mbili za njano baada ya kumfanyia madhambi mara mbili Eden Hazard katika mchezo wa robo fainali wa kombe la FA dhidi ya Chelsea ulioisha kwa Manchester United kulala kwa bao 1-0 la kipindi cha pili la kiungo Ng'olo Kante.
Taarifa iliyotolewa na FA imesema Herrera amefungiwa mechi mbili badala ya moja kama sheria zinavyoagiza hii ni kutokana na adhabu hiyo kuwa ya pili kwa kiungo huyo msimu huu.
Sasa hii ina maana kwamba Herrera ataungana na Zlatan Ibrahimovic kuikosa michezo miwili ya ligi kuu England dhidi ya Middlesbrough na West Bromwich.Ibrahimovic alifungiwa mechi tatu kwa kosa la kumchapa kiwiko Tyrone Mings wa Bournemouth.
0 comments:
Post a Comment