.London,England.
Chama cha soka nchini England FA leo ijumaa.kimemfungia mchezo mmoja pamoja na kumpiga faini ya £20,000 mshambulizi wa Chelsea Diego Costa kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu alivyovionyesha katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Everton mwezi Machi.
Katika mchezo huo uliopigwa Goodison Park na Chelsea kulala kwa mabao 2-0 Costa,27 alitolewa dimbani dakika ya 84 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kufuatia kuonyesha umwamba na kiungo wa Everton Gareth Barry.
0 comments:
Post a Comment