728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 01, 2016

    KUELEKEA EL CLASICO JUMAMOSI:DECO AWAAMBIA REAL MADRID UKWELI UNAOUMA

    Barcelona,Hispania.

    Wakati joto la mchezo wa El Clasico kati ya Barcelona na Real Madrid likizidi kupanda,tambo,majingambo na utani wa hapa na pale vimeendelea kushika kasi.

    Nyota wa zamani wa Barcelona na Ureno Deco de Souza amesema ni mchezaji mmoja tu wa Real Madrid ndiye mwenye uwezo wa kupata namba katika kikosi cha sasa cha Barcelona.

    Akifanya mahojiano na gazeti la Ara la Catalunya,Deco,40 amemtaja kiungo Luka Mondric kuwa ndiye mchezaji pekee wa Real Madrid anayeweza kupata namba katika kikosi cha Los Blaugrana.

    Amesema "Ni Mondric pekee.Aina yake ya uchezaji inaendana vilivyo na Barcelona.Ukimtazama anavyocheza utadhani unawatazama Andres Iniesta na Xavi Hernandez. Ronaldo,Benzema na Bale hawana nafasi Barcelona.

    Barcelona na Real Madrid zitaumana kesho jumamosi Nou Camp katika muendelezo wa michezo ya ligi ya La Liga.

    Picha ya Chini ni kiungo Luka Mondric

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA EL CLASICO JUMAMOSI:DECO AWAAMBIA REAL MADRID UKWELI UNAOUMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top